God Graciously hear us

May your angles Lord be constantly bringing these prayers before you

Grant Us your Peace always for you said in Phil 4:4-7

4Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice! 5Let your gentleness be evident to all. The Lord is near. 6Do not be anxious about anything, but in everything, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God. 7And the peace of God, which transcends all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.

Friday, April 20, 2018

Utuinue na kutuimarishe ee Bwana

Utuinue na kutuimarishe ee Bwana sisi Kanisa lako

Twakusihi Mungu kwa huruma yako ee Mungu, tuwezeshe kujitoa kwako kuwa sadaka hai, takatifu na inayokupendeza Mungu, ambayo ndio ibada yetu ya kiroho. Wala tusiige tabia na mienendo ya dunia hii bali tubadilishwe, nia zenu zifanywe kuwa mpya, ili tupate kuwa na hakika ni nini mapenzi yako Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pako na makamilifu. Rum 12:1-2

Utujalie ee Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu,roho ya hekima na ya mafunuo tupate kukufahamu zaidi.  macho ya mioyo yetu yaangaziwe ili tupate kujua tumaini tuliloitiwa, na tutambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu;  na tuu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu  ambayo uliitumia ulipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, ukamweka akae mkono wako wa kulia katika enzi yako mbinguni.  Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. Nawe Mungu umeweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na ukamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa,  ambalo ni mwili wake, nalo limejawa na yeye ambaye hujaza kila kitu kwa kila njia. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo. Efe 1:17-23


Na kupitia katika hiyo  neema na utume tuliokirimiwa na wewe Mungu kwa njia ya Yesu kristo Tupate  kuyaweza yote mambo yote katika wewe ututiaye nguvu. Rum 1,Fil 4


No comments:

Post a Comment