God Graciously hear us

May your angles Lord be constantly bringing these prayers before you

Grant Us your Peace always for you said in Phil 4:4-7

4Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice! 5Let your gentleness be evident to all. The Lord is near. 6Do not be anxious about anything, but in everything, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God. 7And the peace of God, which transcends all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.

Monday, September 28, 2015

Unitakase na unilinde Ee Bwana,kiburi kisinitawale

Ee Mungu,Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.
Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.
Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Zab 19:7-14

Thursday, September 10, 2015

Yesu Mfalme wangu,ufalme wako uje ndani yangu.

Mungu baba naomba unisamehe kwa kuruhusu wakati wowote kiti cha enzi cha uovu/shetani kuingia ndani yangu kwa kujua au kutokujua,ninaomba unitakase kwa damu yako Yesu na ninakivunja hicho kiti,ninakipindua na kukukaribisha Yesu uingie kuchukua nafasi ya utawala katika maisha yangu.Njoo ufanyike mfalme wangu,mwamuzi wangu na mtunga sheria wangu.Ee Yesu ufalme wako uje,haki yako ifanye makao yake daima ndani yangu niweze kumiliki na kutawala pamoja nawe Yesu

Katika Jina la Yesu nakataa kila ushirika na ulimwengu wa giza na mikataba na maagano yote niliyoingia nayo naivunja na kubatilisha kwa Jina la Yesu,Napokea agano la Damu ya Yesu katika maisha yangu kama agano kuu lenye kusimamia maisha yangu,Asante Yesu kwa Kunikomboa na kunipatanisha na Mungu na kunifanya mwenye haki wa Mungu.Uhimidiwe Mungu Mkuu unayestahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.


Friday, May 22, 2015

Prayer Points

Maombi haya nilipata kuomba wakati naombea ndoa na watoto,ni vizuri tukishirikishana pia pamoja.

 Katika ndoa
1.Kuomba Mungu atuinue katika ndoa kwenda kiwango kingine(katika ulinzi,hekima nk.) kadiri anavyotuinua katika maeneo mengine ya maisha.(utukufu hadi utukufu)

2.Kuomba kuwa na moyo wa shukrani na wenye kuridhika(grateful and appreciative heart)


Kwa watoto
 1.Kuombea character development ya watoto,Mungu aondoe visivyofaa vyote.Hapa ni vizuri tukiombea:
-Kuondoa watu wasio sahihi katika maisha na makuzi yao na kujiunganisha na watu sahihi watakaolea kusudi la Mungu ndani yao
-Kuomba walindwe na uovu na uasi na kila pando asilolipanda Mungu lingolewe ndani yao
-Kusema na nafsi zao kwa kuwataja majina kuwa ziukatae uovu na kukubali lililo jema katika ufahamu na mioyo yao;wapende haki na wadumu katika upendo
-Kupanda Neno la Mungu ndani yao kwa kuwatamkia katika maombi mistari ya Neno la Mungu mfano Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako,kwa roho yako,akili yako na kwa nguvu zako zote
-Kuomba Mungu afunulie wazazi tuweze kujua wito na karama za Mungu ndani ya watoto wetu ili tushirikiane na Mungu katika kuwepeleka mahali sahihi kukuza na kuimarisha karama zao na makusudi ya Mungu yakathibitike kwa wakati wake katika maisha yao.

Note: Wakati naombea hivyo nikapata kutafakari kuwa matatizo mbalimbali tunayoyapata mfano changamoto za wasaidizi wa ndani ni kwa sababu hatuombei ndoa zetu na watoto wetu kwa kina kwani tukiombea maeneo hayo kwa kina Mungu ataleta watu sahihi  na wala sio wa kuleta uharibifu.

Mimi nimejifunza kitu kweli hapo katika tafakari maaana nilikuwa tu naomba nipate mtu mzuri wa kunisaidia kazi kumbe nilipaswa kupanua wigo wa maombi yangu kuombea kwa kina ndoa na watoto pia. Mungu Mwema na atubariki sote.