15 Mungu tunaomba utujalie kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wako, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wako katika utu wa ndani.
16 Kristo akae mioyoni mwetu kwa imani tukiwa na shina na msingi katika upendo;
17 ili tupate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
18 na kuujua upendo wako Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, tupate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
19 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
20 naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. Efe 3:15-20
No comments:
Post a Comment