Mungu baba naomba unisamehe kwa kuruhusu wakati wowote kiti cha enzi cha uovu/shetani kuingia ndani yangu kwa kujua au kutokujua,ninaomba unitakase kwa damu yako Yesu na ninakivunja hicho kiti,ninakipindua na kukukaribisha Yesu uingie kuchukua nafasi ya utawala katika maisha yangu.Njoo ufanyike mfalme wangu,mwamuzi wangu na mtunga sheria wangu.Ee Yesu ufalme wako uje,haki yako ifanye makao yake daima ndani yangu niweze kumiliki na kutawala pamoja nawe Yesu
Katika Jina la Yesu nakataa kila ushirika na ulimwengu wa giza na mikataba na maagano yote niliyoingia nayo naivunja na kubatilisha kwa Jina la Yesu,Napokea agano la Damu ya Yesu katika maisha yangu kama agano kuu lenye kusimamia maisha yangu,Asante Yesu kwa Kunikomboa na kunipatanisha na Mungu na kunifanya mwenye haki wa Mungu.Uhimidiwe Mungu Mkuu unayestahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment